Bingwa wa ligi kuu ya vijana (under 20) Mtibwa Sugar jana walishuka uwanjani na katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Simba katika uwanja wa uhuru na vijana hao wa wana tam tam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 0-1 dhidi ya Simba sc.

Goli hilo  la wana tam tam lilipatikana dakika ya 44′ kupitia kwa mshambuliaji wake  Omary Marungu akimalizia pasi ya Richard William  Mwamba.

Baada ya matokeo hayo wana tam tam wamekusanya pointi pointi  16 katika michezo 8 ya kundi B na wanaongoza kundi hilo huku wakiwa wamebakiwa na michezo miwili ili kukamilisha ratiba ya makundi.

Kocha wa kikosi cha timu ya vijana Awadh Juma aliuambia mtandao wa www.mtibwasugar.co.tz kuwa kila mchezo kwao ni muhimu kwasababu wanataka kulinda ubingwa.

“kila mchezo kwetu ni muhimu tunataka kushinda kila mchezo kwasababu sisi ndo tunashikilia ubingwa huu tunatakiwa tucheze kwa heshima na taadhari” Awadh

Kikosi cha Mtibwa under 20 dhidi ya Simba

Razack Shekimweli, Nicskon Mosha, Omary Manga, Omary Jumanne/Said Kazi, Abdulsattar Sabri Caminero Kapilima, Omary Khamis ”Buzungu”, Frank Kahole, Nassor Kiziwa/Yassin Mohamed, Joseph Mkele, Richard Mwamba/Hussein Kombo, Omary Marungu

Comments are closed.