Mtibwa Sugar Jumatatu hii ya tarehe 26/04/2021 watashuka dimbani kuwakaribisha Polisi Tanzania katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro .

Hadi sasa Mtibwa Sugar imekusanya pointi 28 katika michezo 26 ikiwa nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu bara huku Polisi wao wakikusanya pointi 34 katika michezo 27.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta meneja wa kikosi cha wana tam tam David B’goya kuelekea mchezo huo

“tumejiandaa vizuri nina imani tutafanya vizuri katika mchezo huo wa Jumatatu tunataka kushinda kila mchezo na nia ipo na hali ipo  , pili ninawaomba wana Morogoro na wapenzi na mashabiki wote wa Mtibwa waje kwa wingi Jamhuri kutupa support siku ya Jumatatu” David B’goya

Aidha David B’goya alizungumzia hali ya kikosi cha wana tam tam kwa upande wa afya za wachezaji wake kuelekea mchezo huo dhidi ya Polisi

“mpaka sasa hatuna majeruhi wapya bali mchezaji pekee anaye umwa ni Saleh Khamis Abdallah majeruhi wa muda mrefu nina imani waliobaki watatuwakilisha vizuri na Kihimbwa tayari kapona ikimpendeza mwalimu  atamtumia” David B’goya

Comments are closed.