Kikosi cha timu ya vijana Mtibwa Sugar jana kilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa ufunguzi wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20 (Under 20 Premier League) na kimepoteza 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Wana tam tam walikuwa wa kwanza kupata goli baada ya mchezaji wa Tanzania Prisons Kaburu Mazanda kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na beki wa kulia wa wana tam tam Nickson Mosha dakika ya 12.

Tanzania Prisons walipata magoli yao kupitia kwa Kelvin Christom 46′ na Joseph Frank 74′ katika dakika  45′ za kipindi cha pili kipindi cha pili cha mchezo.

Timu ya vijana ya Wana tam tam wataendelea kusalia jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo unaofuata ambao watacheza dhidi ya Ihefu katika uwanja wa Highland Estates Jumatano ya tarehe 17/03/2021.

Wana tam tam wapo kundi B katika ligi hiyo ya vijana na timu nyingine ambazo zipo kundi hilo ni KMC (Dar es salaam), Simba Sc (Dar es salaam), Ihefu (Mbeya), Mbeya City (Mbeya) na Tanzania Prisons (Rukwa).

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha wa kikosi cha timu ya vijana Vicent Barnabas ili kujua hali ya kikosi chake baada ya mchezo wa jana

“timu bora jana imepoteza ila nina imani tutaendelea kupambana ili tuweze kufuzu hatua ya 8 bora, sisi ni mabingwa mara mbili mfululizo hivyo kila timu inayokutana nasi inajitoa kwa nguvu zake zote kwasababu wanajua wanapambana na bingwa mtarajiwa, tunatakiwa tuonyeshe kuwa sisi kuwa mabingwa mara mbili mfululizo hailikuwa jambo la kubahatisha ni uwekezaji mkubwa hivyo vijana wanatakiwa wakapambane mchezo ujao nina imani tutatoka hapa na pointi za Ihefu”Barnabas

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichocheza dhidi ya Prisons

Razack Shekimweli, Nickson Mosha, Said Kazi Salum, Nassry Kombo, Omary Jumanne/Abdulsattarsabri Caminero Kapilima, Frank Kahole, Jabir Masumbuko, Joseph Mkele/Hussein Kombo, Yassim Muhdin, Nassor Kiziwa/Omary Marungu, Richard Mwamba

Comments are closed.