Leo (Jumatano) kikosi cha Mtibwa Sugar kimeshuka uwanjani kucheza mchezo wake wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Biashara United katika mchezo uliochezwa saa nane mchana, mchezo huo umemalizika kwa sare ya 0-0 na Wana tam tam wamefikisha pointi 24.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu Hitimana Thierry  wa kikosi cha wana tam tam ambaye leo ndo alikuwa anaongoza kikosi cha Mtibwa katika mchezo huo na amesema wanaendelea kutengeneza timu kuelekea katika ubora wetu.

tumepata sare lakini tunazidi kuimarika kwa jinsi tulivyocheza nina imani  mchezo ujao tutafanikiwa tulikuwa na shida katika safu ya ulinzi  hivi karibuni kuruhusu magoli rahisi lakini kwa sasa tatizo hilo tumelimaliza unaona jinsi kijana huyu Masenga ana cheza ameleta kitu katika timu yetu” Hitimana

Baada ya mchezo waleo wana tam tam wataendelea kubakia uwanja wa nyumbani (Jamhuri) kuwakaribisha Gwambina tarehe 7/03/2021 katika mchezo wa ligi kuu bara.

Kikosi cha wana tam tam leo dhidi ya Biashara

Abuutwalib Mshery, Salum Kanoni Kupela, Issa Rashid Issa, Jofrey Luseke Kiggi, Jamal Masenga, Baraka Majogoro, Ismail Aidan, Ally Yusuf Makarani, Riphat Khamis, Abal Kassim Khamis/Kelvin Sabato Kongwe, George Makanga/Haroun Chanongo

Comments are closed.