Leo klabu ya Mtibwa Sugar walikuwa uwanjani (Jamhuri,Morogoro) kuwakaribisha JKT Ruvu katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Dakika 90′ zimemalizika kwa sare ya kufungana 2-2 , Mtibwa walipata magoli yao kupitia kwa Abal Kassim Khamis 5′ na Issa Rashid Issa (Baba Ubaya) 90′ huku JKT Ruvu wakipata magoli yao kupitia kwa Danny Lyanga 17′ na 27′.

Baada ya dakika 90′ kukamilika timu zote mbili iliamuliwa ipigwe mikwaju ya penati na JKT wamefanikiwa kufuzu kwa kufanikiwa kufunga mikwaju yote mitano huku Mtibwa wakifanikiwa kupata kufunga mikwaju minne na kukosa 1, hivyo JKT Ruvu wamefuzu kwa mikwaju 4-5.

Baada ya mchezo wa leo wana tam tam wataendelea kusalia katika uwanja wa nyumbani (Jamhuri) kuwakaribisha Biashara katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) utakaochezwa tarehe 4/03/2021.

Comments are closed.