Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Mtibwa Sugar, leo wametoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ihefu walikuwa wa kwanza kupata goli lilofungwa kupitia kwa mshambuliaji wao Issa Rashid Ngoah 13′  na Mtibwa walisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao matata aliyejiunga nao dirisha dogo Kelvin Sabato Kongwe 38′.

Baada ya mchezo wa leo wana tam tam watasafiri hadi Dar es salaam kwa ajili ya kucheza mchezo mwingine wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Yanga tarehe 20/02/2021.

Kikosi cha leo dhidi ya Ihefu:

Shaaban Hassan Shaaban ”Kado”, Hassan Ramadhani Kessy/Awadh Salum Juma, Issa Rashid baba ubaya”, Jofrey Luseke Kiggi, Dickson Daud Mbeikya,  Juma Nyangi Ganambali, Riphat Khamis Msuya/Ismail Aidan Mhesa, Ally Yusuf Makarani,Kelvin Sabato Kongwe, Abal Kassim Khamis, George William Makanga

Comments are closed.