Bingwa mtetezi wa  kombe la Mapinduzi , Mtibwa Sugar leo imecheza mchezo wake wa kwanza wa Mapinduzi Cup 2021 dhidi ya Chipukizi United Fc katika uwanja wa Amani.

Dakika 45′ za kipindi cha kwanza zimemalizika  0-0 na Wana tam tam walifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Salum Kanoni na kumuingiza Ibrahim Ahmada Hilika na mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Mtibwa sababu yaliongeza kasi ya mashambulizi na Wana tam tam walifanikiwa kufunga kupitia kwa Hilika dakika ya 58′ akipokea pasi ya winga George Makang’a, goli hilo limefanikiwa kuipa Mtibwa ushindi 1-0.

Aidha kiungo mkabaji wa wana tam tam Juma Nyangi Ganambali amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mchezo leo na amezawadiwa hundi ya shilingi laki mbili, baada ya mchezo wa leo wana tam tam watacheza mchezo wao wa pili dhidi ya Simba siku ya Jumamosi ya Desemba 9, saa 2;15 usiku ili kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2021.

KIKOSI CHA LEO DHIDI YA CHIPUKIZI.

Shaaban Hassan Shaaban, Salum Kanoni/Hilika, Omary Sultan, Dickson Daud, Geofrey Luseke, Juma Nyangi, Ismail Mhesa/Riphat Khamis, Abal Kassim Khamis/Mohamed Abdallah Rashid, Jaffary Kibaya, Ally Mkarani, George Makang’a

Comments are closed.