Leo (Jumamosi) kikosi cha Mtibwa Sugar kimeshuka uwanjani kucheza mchezo wake wa mzunguko wa kumi na nane  wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi.

Wana tam tam leo wamepoteza mchezo 2-0 goli zote zikifungwa kipindi cha pili cha mchezo,Ruvu Shooting wamefunga goli lao la kwanza dakika ya 80′ baada ya mchezaji wa Mtibwa Sugar Baraka Majogoro kujifunga katika harakati za kuokoa mpira ulipigwa na David Richard, na Ruvu walipata goli lao la pili kupitia kwa Frank Ikobela dakika ya 85′.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha msaidizi Vicent Barnabas wa kikosi cha wana tam tam ambaye leo ndo alikuwa anaongoza kikosi cha Mtibwa katika mchezo huo na amesema kuwa wamepoteza na sasa maandalizi yao kutetea ubingwa wa kombe la Mapinduzi.

tumepoteza mchezo muhimu sana tulikuwa tunahitaji pointi tatu ili kuendelea kutafuta pointi za kufikia lengo letu la kuwa timu za juu katika msimamo wa ligi kuu bara, tumepoteza na sasa nguvu zetu tunazielekeza katika kutetea ubingwa wa Mapinduzi Cup ambao bado tunaushikilia sisi” Barnabas

Kikosi cha wana tam tam leo dhidi ya Ruvu Shooting

Shaaban Kado/Hassan Kessy/Haroun Chanongo, Issa Rashid, Dickson Job, Dicskon Daud, Baraka Majogoro, Ismail Aidan/Abdul Yusuf Haule, Ally Yusuf Makarani, Riphat Khamis/George Mkanga, Jaffary Kibaya, Abal Kassim Khamis

Comments are closed.