Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Ettiene Ndairagije leo Disemba 29,2020  ametaja kikosi cha timu taifa  ya Tanzania chenye jumla ya majina 30.

Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuingiza wachezaji watatu katika kikosi hicho cha wachezaji 30, wachezaji waliochaguliwa ni kipa  Abuutwalib Hamidu Mshery , kiungo wa chini Baraka Gamba Majogoro na beki wa kati Dickson Nickson Job.

Wachezaji wengine walio itwa ni Aishi Manula (Simba), Juma Kaseja (KMC), Dan Mgore (Biashara), Shomari Kapombe (Simba), Israel Mwenda (KMC), Edward Manyama (Namungo),Yassin Mustapha (Young Africans), Bakari Mwamnyenyeto (Yanga), Agrey Morris  (Azam), Erasto Nyoni (Simba) na Carlos Protas (Namungo).

Wengine ni Said Ndemla (Simba), Yusuf Mhilu (Kagera), Ayoub Lyanga (Azam), Feisal Salum, Rajab Athuman (Gwambina), Ditram Nchimbi (Young Africans), John Bocco (Simba), Deus Kaseke (Young Africans), Lukas Kikoti (Namungo), Farid Mussa (Young Africans), Adam Adam (JKT Tanzania), Abdulrazack Hamza (under 20 Mbeya City),  Khelfinie Salum (Under 20 Azam), Samwel Jackson (Under 20 Ihefu), Omari Omari (under 17) na Pascal Gaudance (under 20 Azam).

Kikosi hicho kilichotajwa leo kitaingia kambini January 1,2021  kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya CHAN 2021 (Wachezaji wanocheza ligi ya nyumbani)  na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya  CONGO DRC.

Wachezaji wote waliotajwa kutoka katika kikosi cha Mtibwa Sugar wanacheza  idara ya ulinzi (Defence) na Mtibwa Sugar ni kati ya timu ambazo zinafanya vizuri katika idara hiyo hadi sasa baada ya kuruhusu magoli  10 tu katika michezo 17 na kuwa timu ya tatu iliyo ruhusu goli chache nyuma ya Simba na Yanga huku kipa wake Abuutwalib Mshery akiwa na cleen sheets 9 katika michezo 15 aliyocheza ya ligi kuu bara (Vodacom Premier League).

Comments are closed.