Mtibwa Sugar imeanza safari ya kuusaka ubingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup kwa kuwachapa Geita Gold ya mkoani Geita goli moja kwa bila (1-0).

Dakika 45′ za kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0 na wana tam tam  wali ingia kipindi cha pili kwa kasi  kubwa sana na kufanikiwa kupata goli mapema dakika ya 47′ kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji Ismail Aidan Mhesa aliyepiga shuti kali lililozaa goli.

Wana tam tam wamefuzu hatua ya raundi ya nne timu nyingine zilizofuzu ni Namungo ambao waliwafunga Green Worriers 2-0, Simba walishinda 5-0 dhidi ya Maji Maji na Yanga wamefuzu baada ya Singida United kushushwa madaraja mawili na kukosa hadhi ya kucheza kombe la shirikisho.

KIKOSI CHA MTIBWA

Abuutwalib Mshery/Shaaban Hassan, Hassan Kessy, Issa Rashid, Dickson Daud, Dickson Job, Baraka Majogoro, Haroun Chanongo, Awadh Salum/Kassim Khamis, Jaffary Kibaya, Riffat Khamis/Onesmo Mayaya, Ismail Aidan

Kikosi cha wana tam tam kinaendelea na maandalizi yake kujiwinda na mchezo ujao wa ligi kuu bara mzunguko wa 18  dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa January 2,2021 katika uwanja wa Mabatini , Mlandizi.

Comments are closed.