Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Mtibwa Sugar, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Tanzania ya jijini Dodoma katika mchezo wa ligi kuu bara (TPL) uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Goli la Mtibwa Sugar limefungwa na mshambuliaji wake hatari Riphat Khamis Msuya katika dakika ya 42′ ya kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka kwa beki wa kushoto Issa Rashid “Baba Ubaya”.
Baada ya ushindi wa leo wana tam tam wamefikisha pointi 22 baada ya kucheza michezo 16 ya ligi kuu bara (TPL) na mchezo unaofuata wa wana tam tam utakuwa dhidi ya Dodoma Jiji Fc tarehe 23/12/2020 katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kikosi cha leo:
Abuutwalib Mshery, Salum Kanoni “mbavu kunesa”, Issa Rashid “baba ubaya”, Jofrey Luseke Kiggi, Dickson Nickson Job, Baraka Gamba Majogoro, Salum Kihimbwa/Awadh Salum, Ally Makarani, Riphat Khamis/Ismail Mhesa, Ibrahim Ahmada “Hilika”, Juma Nyangi/Dickson Daud