Mtibwa Sugar inataraji kucheza mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Mbeya City Jumamosi hii ya tarehe 28/11/2020 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kikosi cha Mtibwa Sugar chini ya kocha Vicent Barnabas tayari kimefika jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi hii na mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta Vicent Barnabas kuzungumzia mchezo huo.

“ni kweli tayari tumefika Mbeya tangu jana usiku kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi kila mchezaji tuliyesafiri nae yuko salama nina imani morali tuliyo nayo hapa itatupa pointi tatu ingawa najua mchezo hautakuwa rahisi, Baraka Majogoro tulimkosa katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi sababu alikuwa ana kadi tatu za njano anarejea, wachezaji wengine ambao wataukosa mchezo huu kutokana na kuumwa ni Saleh Khamis, Awadh Salum,  Said Mohamed , George Makanga , Salum Kanoni nina imani waliobaki watawakilisha vizuri’‘ Barnabas

Wana tam tam hadi sasa wamecheza michezo 12 na kukusanya pointi 12 huku Mbeya City wao wakiwa wamekusanya pointi 10 katika michezo 12.

Comments are closed.