Bingwa wa ligi kuu bara mara mbili, Mtibwa Sugar Ijumaa hii ya tarehe 20/11/2020 watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Mtibwa Sugar chini ya Vicent Barnabas imeanza safari leo asubuhi kuelekea mkoani Rukwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).

Hadi sasa Mtibwa Sugar imekusanya pointi 11 katika michezo 10 ikiwa nafasi ya 12 huku Tanzania Prisonons wakiwa nafasi ya 8 baada ya kukusanya pointi 15 katika m ichezo 10.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta meneja wa kikosi cha wana tam tam David B’goya kuelekea mchezo huo

“tuko safarini kuelekea Rukwa kwa ajili ya mchezo huo wa Ijumaa kila kitu kiko sawa tunaendelea vizuri tuendelee kumuomba mwenyezi Mungu  tufike salama kwa ajili ya mchezo huo wa Ijumaa” David B’goya

 

Comments are closed.