Baada ya Mtibwa Sugar  kupoteza mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Kagera Sugar  1-0 watakuwa uwanjani siku ya Alhamisi ya tarehe 5/11/2020 kuwakaribisha Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro Mjini, kiingilio katika mchezo huo kitakuwa shillingi 3,000/= .

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz  umemtafuta kocha Vicent Barnabas kuelekea mchezo huo dhidi ya Coastal Union

“Coastal Union wana timu nzuri yenye vijana wengi mno wenye vipaji nina imani tutakutana na timu nzuri na sisi tutapambana tuweze kuibuka na ushindi katika mchezo huo, ninawaomba wana Morogoro waje kwa wingi uwanjani waje waipe support timu yao, nina imani support yao itatupa nguvu na kuweza kuibuka na ushindi” Barnabas

Hadi sasa Mtibwa Sugar iko katika nafasi ya 11 katika msimamo baada ya kucheza mechi 9  na kukusanya mechi 11 huku  Coastal Union ikiwa nafasi  14 baada ya kukusanya pointi 9 katika michezo 9.

Comments are closed.