Bingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar jana wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar  katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri,Morogoro.

Dakika 45′ za kwanza zili isha 0-0 na kipindi cha  pili kilikuwa bora sana kwa Wana tam tam walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kufika mara nyingi katika goli la Azam.

Mtibwa chini ya Vicent Barnabas walifanya mabadiliko (substitution) kwa kuwatoa Ibrahim Ahmada ”Hilika” na kumuingiza Jaffary Kibaya  dakika ya 45′ na dakika ya  54′ walimtoa Haruna Chanongo na kumuingiza Ismail Aidan Mhesa na mabadiriko hayo yalikuwa ya faida sana kwa Mtibwa Sugar baada ya kufanikiwa kupata goli kupitia kwa Jaffary Kibaya aliyefunga dakika ya 62′ kwa shuti kali lka mbali.

Baada ya kufanikiwa kupata goli hilo Vicent Barnabas alifanya mabadiriko kwa kumtoa Salum Kihimbwa na kumuingiza Dickson Daud kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.

Mchezo ufuatao wana tam tam watasafiri kuelekea mkoani Kagera kucheza dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumapili ya tarehe 1/11/2020.

KIKOSI :

Abuutwalib Mshery, Salum Kanoni, Issa Rashid Issa “Baba Ubaya”, Jofrey Luseke Kigi, Dickson  Job,  Baraka Gamba Majogoro, Awadh Salum Issa, Ally Makarani, Ibrahim Ahmada ”Hilika”/Jaffary Salum Kibaya, Salum Kihimbwa/Dickson Daud, Haruna Chanongo/Ismail Mhesa

Comments are closed.