Kikosi cha wana tam tam kimefanikiwa kutoa nyota 6 wana unda kikosi cha timu ya taifa ya vijana Tanzania chini ya umri wa miaka 20 (Ngoro ngoro Heroes).

Wachezaji walio itwa katika kikosi hicho kutoka Mtibwa ni kipa Razack Shekimweli, Jofrey Kiggi Luseke, Steven Burugu, Joseph Mkuwa Mkele, Frank George Kahole na Riffat Msuya.

Wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa chini ya miaka 20 (Under 20) chenye nyota 50 kwa ajili ya mchujo wa awali.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa timu za vijana Vicent Barnabas juu ya nyota hao kuitwa timu ya taifa.

kiukweli ni nzuri kwa timu yetu inaonyesha jinsi gani tumewekeza kwa vijana na matunda yake ni kama haya kulitumikia taifa na kwa upande wa vijana wetu inawatia morali kuendelea kupambana kwa ajili ya kesho yao” Barnabas

Comments are closed.