Jumatatu ya tarehe 26/10/2020 wana tam tam watakuwa uwanjani kuwakaribisha Azam Fc katika uwanja wetu wa  nyumbani Jamhuri,Morogoro katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).

Wana tam tam wanaendelea na mazoezi yao katika kambi yao iliyopo kati kati ya mashamba ya miwa Turiani, Morogoro, Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha Vicent Barnabas juu ya mchezo ujao dhidi ya Azam.

”tunaendelea na mazoezi yetu kwa ajili ya mchezo huo ila najua Azam ni wazuri ila sisi tunahitahi pointi tatu muhimu ili tuweze kukaa sehemu nzuri katika msimamo, nina imani morali tuliyonayo hii ikiendelea hivi hivi  tutashinda mchezo wetu kwasababu kila mchezaji morali iko juu sana” Barnabas

Mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) timu hizi kukutana Mtibwa Sugar walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0  katika uwanja wa CCM,Gairo, goli lilifungwa na Issa Rashid“Baba ubaya” kwa kona ya moja kwa moja

 

Comments are closed.