Bingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar jana wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo katika mchezo wa ligi kuu bara uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Wana tam tam walifanikiwa kufunga goli hilo dakika ya 76′ kupitia kwa Salum Ramadhani Kihimbwa kwa mkwaju wa penati baada ya Carlos Protas kumkwatua Kihimbwa ndani ya penati box.

Kikosi kilichocheza jana dhidi ya Namungo

Abuutwalib Mshery, Salum Kanoni, Omary Sultan Hassan, Jofrey Luseke Kigi, Dickson Nickson Job, Baraka Gamba Majogoro, Joseph Mkuwa Mkele/Haruou  Chanongo, Awadh Salum Juma, Ibrahim Hamad ”Hilika”/Jaffary Kibaya, Salum Ramadhani Kihimbwa/Dickson Daud, Ally Makarani

Baada ya matokeo ya jana wana tam tam wamefikisha pointi 8 katika michezo 7 ya ligi kuu bara (Vodacom Premier League) na mchezo ujao watacheza dhidi ya Azam fc tarehe 26/10/2020 katika uwanja wa nyumbani Jamhuri,Stadium.

Comments are closed.