Kikosi cha Mtibwa Sugar jana kilipoteza mchezo wake wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Gwambina ya jijini mwanza kwa goli 2-0. Magoli ya Gwambina yalifungwa na Yusuph Lwege 20′ na Meshack Mwamita 88′

Baada ya matokeo hayo kikosi cha wana tam tam kimebaki na pointi tano kikiwa nafasi ya ya 13 katika msimamo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).

Kikosi kilichocheza dhidi ya Gwambina Fc

Shaaban Kado, Salum Kanoni, Omary Sultan Hassan, Jofrey Luseke Kigi, Dickson Job, Baraka Gamba Majogoro, Awadh Salum Juma, Juma Nyangi/Abdul Yusuf Haule, Jaffary Kibaya/Haruna Chanongo, Riphat Khamis, Joseph Mkele/Ismail Mhesa

Wana tam tam leo wako njiani wakirejea kutoka jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Namungo utakaochezwa tarehe  19/10/2020.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha msaidizi wa kikosi hicho Vicent Barnabas Salamba juu ya mchezo huo wa jana

”tumepoteza mchezo ambao hatukutakiwa kupoteza inauma ila tunajiandaa na mchezo ujao dhidi ya Namungo tutakuwa nyumbani  tutarekebisha pale tunapokosea na nina imani tutaibuka na pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo siku ya Jumatatu” Barnabas

Comments are closed.