Kikosisi cha Wana tam tam chini ya kocha  Zubeir Katwila kinaendelea na mazoezi yake katika uwanja wake wa Manungu Complex kikijiandaa na mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Gwambina utakaochezwa,Gwambina Stadium Mwanza tarehe 15/10/2020.

Wachezaji wote wanaendelea na mazoezi isipokuwa wachezaji watano ambao ni Saleh Khamis Abdallah (kisigino) ana majeraha ya muda mrefu, Abubakary Ame (Luiz) aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Geita Gold , Salum Ramadhani Khimbwa aliumia enka katika mchezo wa ligi dhidi ya Young fricans na George William Makanga anaye endelea na matibabu.

Mchezaji mwingine anayekosekana katika mazoezi hayo ni Dickson Nickson Job ambaye yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wakijiandaa na mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Burundi.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha msaidizi wa kikosi cha Mtibwa Vicent Barnabas Salamba juu ya maandalizi ya mchezo huo wa Alhamisi.

“kila mchezaji ana hali nzuri kiukweli mchezo ujao nina imani tutafanya vizuri kwasababu tumeangalia tumekosea wapi katika mchezo dhidi ya Biashara  na tumerekebisha makosa yetu hivyo basi nina imani mechi ijayo dhidi ya Gwambina tutaibuka na pointi tatu” Barnabas

Comments are closed.