Kikosi cha Mtibwa Sugar kimepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Young Africans 1-0, Young Africans  walifunga goli lao kupitia kwa  beki wao Lamine Moro 61′.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa kikosi cha wana tam tam ambaye leo  alikiongoza kikosi cha Mtibwa katika mchezo huo.

tumepoteza mchezo muhimu sana tulikuwa nyumbani na tulihitahi pointi tatu ili tuendelee kuwa juu katika msimamo , tunaenda kufanya maandalizi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Gwambina’ Katwila

Mchezo ujao Mtibwa Sugar watakuwa uwanjani  dhidi ya Gwambina ya Mwanza na mchezo huo utachezwa katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 04/10/2020

Kikosi cha wana tam tam leo dhidi ya Young Africans

Abuutwalib Mshery, Hassan Kessy, Issa Rashid, Jofrey Luseke, Dickson Job, Baraka Majogoro/AwadhSalum, Boban Zirintusa/Juma Nyangi, Hilika, Joseph Mkele, Haruna Chanongo, Salum Kihimbwa/Riphat Khamis

Comments are closed.