Bingwa wa ligi kuu bara mara mbili, Mtibwa sugar leo wametangaza rasmi kuwa uwanja wao wa nyumbani utakuwa Jamhuri Stadium ambao upo kati kati ya mji wa Morogoro.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz  umemtafuta msemaji wa klabu ya Mtibwa , Thobias Kifaru Ligalmbwike juu ya taarifa hiyo ya kuhamia Jamhuri.

“ni kweli tumeamua kuhamia Jamhuri stadium uliopo kati kati ya mji wa Morogoro, tayari bodi ya ligi wamebariki uamuzi wetu kwa kutuandikia barua rasmi hivyo michezo yetu yote ya kiushindani tutachezea Jamhuri, tunawaomba wana Morogoro watupe sapoti  katika hili kwa kuja kwa wingi uwanjani kutushangilia katika michezo yetu tutakayocheza katika uwanja wa Jamhuri’‘ Kifaru

Aidha msemaji wa  bingwa wa ligi kuu bara mara mbili Thobias Kifaru Ligalambwike amezungumzia mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Young Africans ambao utachezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro

”Vijana wana ari kubwa tuombe morali hii iendelee hadi  siku hiyo ya Jumapili , nimeongea na benchi la ufundi chini ya kocha wetu  mkuu Zubeir Rashid Katwila na wameniambia wako fiti kuwakabili Young muda wowote, kiukweli tunahitaji pointi tatu kutoka kwa Young Africans tumesajili vizuri sana msimu huu hivyo pointi tatu dhidi ya Young Africans ni haki yetu, ninawaomba wana Mtibwa waje kwa wingi washudie burudani ya hali ya juu sana kutoka kwa wana tam tam” Kifaru

Kikosi cha vijana wa Zubeir Katwila kinaendelea na maandalizi yake katika kambi yake iliyopo Turiani katika kuhakikisha kinajiwinda kisawa sawa dhidi ya Young Africans.

Mchezo huo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) Mtibwa Sugar dhidi ya Young Africans utachezwa siku ya Jumapili ya tarehe 27.09.2020 katika uwanja wa Jamhuri kwa kiingilio cha Tsh.10,000

Comments are closed.