Wana tam tam Jumapili hii ya tarehe 27/09/2020  watakuwa wenyeji wa  Young Africans  katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) utakaochezwa katika uwanja wetu wa nyumabani Jamhuri, Morogoro.

Wana tam tam wanaendelea na maandalizi yao katika kambi yao iliyo kati kati ya block za miwa, mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa kikosi cha Mtibwa Sugar Zuber Katwila na kutaka kujua maandalizi ya mchezo huo wa mzunguko wa nne wa ligi kuu bara.

“maandalizi yetu yako vizuri kama unavyo ona wachezaji wote wako vizuri, sina majeruhi yeyote katika kikosi changu hadi sasa kila mchezaji anafanya vizuri mazoezini hivyo atakayekuwa vizuri zaidi hadi siku ya mwisho atacheza mchezo wa mwisho. Yanga ni wazuri lakini tunacheza nyumbani tuna nguvu ya wana Morogoro pia nawa amini wachezaji wangu nina imani tutafanya vizuri sana na kupata pointi tatu” Katwila

Wana tam tam hadi sasa wamekusanya pointi 5 baada ya kucheza michezo mitatu ya ligi kuu bara na hizi zimepatikana kwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili, ikiwa inshika nafasi ya 7 katika msimamo huku Young Africans ikiwa inashika nafasi ya 5 huku ikiwa ina pointi 7 baada ya kushinda michezo miwili na kutoka sare mchezo 1.

Comments are closed.