Bingwa wa kombe la Mapinduzi 2020, Mtibwa Sugar jana walicheza mchezo wao wa 16 katika ligi kuu bara (Vodacom Premier League) na kupoteza 2-0 dhidi ya KMC katika uwanja wa Uhuru.

KMC walipata magoli yao yote mawili kwa kupitia mshambuliaji wao wa kati Salada Lipagwile kipindi cha kwanza  dakika ya 18′ na 41′ kipindi cha kwanza.

KIKOSI CHA MTIBWA 

Shaaban Hassan Shaaban “Kado”, Kibwana Ally Shomary, Issa Rashid Issa”Baba Ubaya”/Omary Sultan, Cassian Ponera Cassian, Abdulhalim Humoud, Awadh Salum Juma/Haruna Chanongo, Ally Makarani, Jaffary Kibaya, Onesmo Mayaya/Riphat Khamais, Salum Kihimbwa

Baada ya mchezo wa jana wana tam tam wamesafiri kuelekea Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Azam Sports Federation Cup (FA) dhidi ya Sahare All Stars ya Tanga.

Mchezo ujao dhidi ya Sahare All Stars utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa wana tam tam (CCM Shabiby Gairo) tarehe 25.01.2020.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta msemaji wa klabu ya Mtibwa Sugar ili kutaka kujua mwenendo wa timu hiyo na maandalizi ya mchezo ujao.

“jana tumepoteza mchezo ila hatujapoteza ligi tunajiandaa kivingine nina uhakika wana tam tam watapenda sana matokeo yanayokuja baada ya kuongea na walimu wetu wamenipa sana moyo sasa kazi iliyopo ni kushinda kombe la Azam Sports Federation Cup kwanza dhidi ya Sahare ya Tanga “ Kifaru

 

Comments are closed.