Bingwa wa Mapinduzi Cup 2020, Mtibwa Sugar kesho watashuka dimbani katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya KMC katika uwanja wa Uhuru, Dar es salaam saa 10:00 jioni.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa kiksoi cha wana tam tam Zubeir Katwila kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).

“KMC ni timu nzuri lakini wajue wanaenda kucheza na timu bora sana ninawaomba wana tam tam waje kwa wingi kuja kutupa sapoti nina imani sapoti yao itatusaidia sisi kuibuka na pointi tatu muhimu” Katwila

Kikosi cha wana tam tam kipo jijini Dar es salaam tangu Jumanne ya tarehe 14.01.2019 baada ya kumaliza michuano ya Mapinduzi Cup 2020 kilisafiri moja kwa moja jijini hadi Dar es salaam.

Wachezaji walio jijini Dar es salaam na kikosi cha wana tam tam ni Makipa  Shaaban Hassan Shaaban “Kado”, Said Mohamed “Nduda” na  Abuutwalib Mshery.

Mabeki ni  Kibwana Shomary, Salum Kanoni Kupela, Issa Rashid Issa “Baba Ubaya”. Cassian Ponera, Dickson Daud Mbeikya, Dickson Job.

Viungo ni Henry Joseph Shindika, Abdulhalim Humoud Mohamed, Awadh Juma Issa “‘Maniche”, Awadh  Salum Juma, Issa Kajia Kigingi, Ally Makarani, Omary Sultan Hassan na Onesmo Mayaya na washambuliaji ni Salum Ramadhani Kihimbwa, Ismail Aidan Mhesa, Haruna Chanongo, Jaffary Kibaya na Riphat Kamis.

Comments are closed.