Kikosi cha timu ya vijana Mtibwa Sugar (under 20) jana kilikuwa uwanjani kikicheza mchezo wake dhidi ya Alliance Football Club katika ligi kuu ya vijana (U 20) na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kikosi cha timu ya vijana ya Mtibwa Sugar chini ya kocha wake Vicent Barnbas Salamba walicheza vizuri kwa kwa kupasiana na kupelekea kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, dakika ya 45+3 za kipindi cha kwanza wanatam tam walifanikiwa kupata penati iliyotokana na beki wa Alliance kumuangusha kiungo mshambuliaji wa wana tam tam Onesmo Justin Mayaya na penati ilifungwa na Abdul Yusuf Haule.

Baada ya kufunga penati ya jana iliyo wahakikishia wana tam tam kufuzu hatua ya robo fainali kwa pointi 16 katika michezo 8, Abdul Haule amefikisha magoli 8 katika hatua ya makundi akiwa kinara wa magoli kwa wana tam tam.

Baada ya mchezo wa jana mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa kikosi cha timu ya vijana Vicent Barnabas Salamba kuhusu mchezo huo

“tumeshinda mchezo muhimu uliotupatia pointi za kwenda hatua ya robo fainali, Alliance wana timu nzuri lakini vijana wangu wamepambana sana na pia namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kumaliza hatua hii salama” Barnabas

Comments are closed.