Kikosi cha timu ya vijana Mtibwa Sugar (under 20) jana kilikuwa uwanjani kikicheza mchezo wake dhidi ya Singida United katika ligi kuu ya vijana (U 20) na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-0.

Magoli ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa jana yamefungwa na Abdul Yusuf Haule aliyefunga dakika ya 4′, 31′ na 44 na magoli mengine yalifungwa na Abubakar Juma 40′ na Jabir Masumbuko 67′.

Baada ya matokeo hayo ya jana wana tam tam wanashika nafasi ya 2 katika kundi B baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 13 huku Ruvu shooting wakiwa wamekusanya pointi 14 na kuongoza kundi.

Mchezo unaofuata timu ya vijana ya wana tam tam watacheza dhidi ya Alliance Football Club katika  mchezo wao wa mwisho wa makundi ili kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali, timu mbili za juu katika kila kundi zitafuzu robo fainali.

Mchezo ujao wana tam tam watacheza dhidi ya Alliance tarehe 2/06/2019 katika uwanja wa Manungu,Morogoro

KIKOSI:

Razack Ramadhani, Kibwana Shomari, Nickson TikeTike, Ramadhani Shemsanga, Jamal Masenga,Frank George/Jabir Masumbuko, Yassin Muhdin, Abubakar Juma, Abdul Haule, Onesmo Mayaya/Nassor Saadun, Nassor Kiziwa/Omar Kusaga

 

 

Comments are closed.