Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili, Mtibwa Sugar, jana walihitimisha msimu wa 2018/2019 kwa sare ya bila kufungana katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Wana tam tam chini ya kocha mkuu  Zuber Katwila walitandaza soka safi kwa uelewano mkubwa sana lakini hawakuweza kufunga goli, Jaffary Kibaya, Ismail Mhesa na Juma Luizio walipata nafasi za kufunga lakini hawakuweza kuzitumia.

Baada ya matokeo ya 0-0 ya jana wana tam tam wamefikisha pointi 50 na kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu bara nyumba ya Simbva, Yanga, Azam na KMC.

Wana tam tam wamefikisha pointi 50 baada ya kushinda michezo 38 na kufanikiwa  kushinda michezo 14, sare 8 , wana tam tam walipoteza michezo 15.

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR:

Benedict Tinocco, Rodgers Gabriel, Issa Rashid Issa, Cassian Ponera, Hassan Isihaka, Henery Joseph, Saleh Khamis Abdallah/Juma Luizio, Ally Yusuf Makarani, Jaffary Kibaya, Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa/Awadh Juma

Comments are closed.