Mabingwa wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20, Mtibwa Sugar , leo wamepoteza mchezo wao wa ligi kuu ya vijana dhidi ya Alliance kwa 3-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba la Nyamagana, Mwanza.

Alliance wamepata magoli yao kupitia kwa Geofrey John 13′ na Ally Bakari 36′ na 57′ kwa mkwaju wa penalty, Wana tam tam wanaendelea kuongoza kundi B wakiwa wamefanikiwa kukusanya pointi 9 katika michezo 4 huku Alliance wakishika nafasi ya pili na pointi 8 katika michezo 4.

Baada ya mchezo wa leo wana tam tam watacheza mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union tarehe 22 katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Baada ya mchezo wa leo mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umefanya mazungumzo na kocha mkuu wa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar .

“tumepoteza mchezo muhimu kwetu, tutaendelea kupambana ili tuweze kupata matokeo katika mchezo ujao dhidi ya Coastal Union, tunaenda Tanga kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali” Vicent Barnabas

Kikosi cha leo:

Razack Shekimweli, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Dickson Job, Jamal Masenga/Jabir  Masumbuko, Fran George, Abubakar Juma/Nassor Kiziwa, Joseph Mkuwa/Onesmo Mayaya, Abdul Haule, Omar Sultan, Aziz Ramadhani

 

Comments are closed.