Mabingwa wa ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Mtibwa Sugar, Leo (Jumanne) jioni wanataraji kushuka dimbani kucheza mchezo wao wa tatu wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 2o dhidi ya Singida United U 20, Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Namfua, mkoani Singida  majira ya saa 10:00 jioni, 14.05.2019.

Kikosi cha wana tam tam tayari kipo mkoani Singida toka juzi (Jumapili) chini ya kocha wake wa timu ya Vijana Vicent Barnabas na kimesafiri na nyota 20 kwa ajili ya mchezo huo.

Wachezaji waliosafiri ni makipa Razack Shekimweli, Khatib Salim na kwa upande wa mabeki ni Kibwana Ally Shomary, Ally Majam, Nickson Kibabage, Dickson Job, Jamal Masenga na Ramadhani Shemsanga.

Viungo ni  Omary Buzungu, Frank “George Kahole “Chumvi”, Abubakar Juma Salum, Joseph Mkuwa, Onesmo Justin Mayaya, Jabir Masumbuko, Omary Sultan na Aziz.

Washambuliaji ni Nassor Seif Kiziwa, Abdul Yusuf Haule, Omary Marungu na Nassor Saadun

Kikosi cha timu ya vijana ya wana tam tam hadi sasa wamecheza michezo miwili na kufanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yote hivyo wana tam tam wamekusanya pointi 6 hadi sasa.

Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Singida United U 20  kikosi cha Mtibwa Sugar U 20 kitasafiri hadi jijini Mwanza kucheza dhidi ya timu ya  Alliance.

 

Comments are closed.