Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili, Mtibwa Sugar, jana wametoka sare ya 2-2 dhidi ya JKT Tanzania, wana tam tam walikuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 34′ kupitia kwa Jaffary Kibaya na Ruvu Shooting walisawazisha kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 63′.

Wana tam tam walirudi kufunga goli la pili kupitia kwa yule yule Jaffari Kibaya dakika ya 65′  na JKT Tanzania walifunga kupitia kwa Abdulrahmana Mussa dakika ya 75′.

Baada ya matokeo hayo ya jana dhidi ya JKT Tanzania, wana tam tam wamefikisha pointi 49′  na kuendelea kushikilia nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu bara (TPL).

Baada ya magoli mawili ya jana yaliyofungwa na Jaffari Salum Kibaya amefikisha magoli 10 katika ligi kuu bara (Tanzania Premier League)

Wana tam tam wanataraji kusafiri kesho (Ijumaa) kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu bara (TPL) dhidi ya Coastal Union na mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili ya tarehe 12.05.2019 , Mkwakwani, Tanga.

Comments are closed.