Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari, Mtibwa Sugar, kesho kikosi chao cha timu ya vijana kinataraji kushuka uwanjani kucheza mchezo wao wa pili dhidi ya Ruvu Shooting katika ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20 (Under 20).

Wana tam tam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 5-1 katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Coastal Union katika ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20.

Magoli ya wana tam tam yalifungwa na Abdul Yusuf Haule aliyefunga mara tatu akipokea pasi mbili za magoli kutoka kwa  Omar Kusaga na goli lingine alilifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Kibwana Ally Shomary kufanyiwa faul ndani ya penalti box.

Omary Kusaga naye alikuwa mmoja wa wafungaji wa magoli alifunga goli dakika ya 64′ akipokea pasi kutoka kwa Abdul Yusuf Haule na goli la mwisho lilifungwa na Onesmo Justin Mayaya 90+1 aliyepokea pasi kutoka kwa Jabir Masumbuko.

Kikosi kilichocheza mchezo huo ni, Razack Shekimweli, Kibwana Ally Shomary, Nickson Clement Kibabage,/Omary Buzungu, Jamal Masenga, Dickson Job, Frank George, Omary Sulatan, Onesmo Mayaya, Abdul Yusuf Haule/Jabir Masumbuko, Omary Kusaga, Nassor Saadun/Nassor Seif Kiziwa

Kesho (Ijumaa) kikosi cha timu ya vijana (Under 20)  chini ya Vicent Barnabas kitashuka dimbani  saa 10:00 jioni katika uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro kucheza mchezo wao wa pili wa ligi kuu ya vijana.

Kiingilio katika mchezo huo ni 1000 kwa watu wazima, na hakutakuwa na kiingilio kwa wanawake na watoto katika mchezo huo wa kesho Mtibwa Sugar u20 dhidi ya Ruvu Shooting u 20.

 

Comments are closed.