Wafalme wa kukuza na kulea vipaji vya soka nchini, Mtibwa Sugar , leo kikosi cha timu ya vijana ya vijana ya Mtibwa Sugar kitakuwa uwanjani kumenyana na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20.

Kikosi cha timu ya vijana cha wana tam tam chini ya kocha wake mkuu Vicent Barnabas Salamba kimepangwa kundi B pamoja na timu za Coastal Union, Alliance, Singida United na Ruvu Shooting.

Viingilio katika mchezo huu itakuwa Tsh.1000 kwa watu wazima  na hakutakuwa na kiingilio (bure) kwa wanawake na watoto chini ya miaka 14 na mchezo huo utachezwa saa 10:00 katika uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha mkuu wa kikosi cha vijana Vicent Barnabas juu ya mchezo huo wa leo dhidi ya Coastal Union.

“nawaomba mashabiki wa Mtibwa Sugar waje kwa wingi uwanjani ili watupe support kufika kwao kwa wingi ndo kutatuongezea morali sisi na kufanikiwa kuibuka na ushindi, nawaomba wana Mtibwa waje kwa wingi”  Barnabas

Comments are closed.