Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili, Mtibwa Sugar , leo wamepoteza mchezo wao wa mzunguko wa 33 wa ligi kuu bara (TPL) dhidi ya Singida United kwa 2-1, Magoli ya Singida yamefungwa na Habib Kyombo dakika 32′  na kwa mkwaju wa penalty dakika ya 90+9 huku goli la wana tam tam likifungwa na Ismail Aidan Mhesa kwa faul  (free-kick) ya moja kwa moja.

Baada ya mchezo wa leo (Singida United V Mtibwa Sugar) mtandao rasmi wa klabu umefanya mahojiano na kocha mkuu wa kikosi cha Mtibwa Sugar Zubeir Shaaban Katwila na amesema mwamuzi hakumudu mpira wa leo.

kiukweli mwamuzi wa leo hakumudu sheria za mpira alizipindisha ili Singida wapate ushindi na kafanikiwa kwa leo lakini tutaendelea kujituma nina imani shirikisho watalifuatilia hili na kupima uwezo wake” Katwila

Wana tam tam wataendelea kubakia katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu bara (TPL) na baada ya kupoteza mchezo huu wa leo dhidi ya Singida United wakiwa wamefanikiwa kukusanya pointi 48 katika michezo 33.

Baada ya mchezo wa leo wana tam tam watarudi katika uwanja wao wa nyumbani (Manungu) kucheza dhidi ya JKT Tanzania siku ya Jumatano ya tarehe 8/05/2018  katika mchezo wa 34 kwa upande wa wana tam tam.

KIKOSI CHA LEO DHIDI YA SINGIDA UNITED

Benedict Tinocco, Salum Kanoni, Issa Rashid, Hassan Is-haka, Dickson Daud, Issa Kajia, Ismail Aidan/Henry Joseph, Ally Makarani, Riphat Khamis/Juma Luizio, Jaffary Kibaya, Haruna Chanongo

Comments are closed.